Posted on: September 16, 2020 Posted by: Kevin Oduor Comments: 0

Polisi Kaunti ya Migori wamefunga hekalu la Legio Maria katika milima ya Got Kwer. Haya yanajiri baada ya vita vikali kuzuka Jumatatu, Septemba 15 baina ya waumini ambapo takriban watu watano walipoteza maisha.

Mzozo mkali uliibuka biaina ya makundi hayo mawili ambapo kikosi cha Adika na msafara wake kilipigwa mawe na kile cha Papa Laurence Ochieng’ Kalul na kuwalazimu polisi kuingilia kati ili kutuliza hali. Katika patashika hiyo watu watu watano walifariki dunia papo hapo huku wengine akiwemo kiongozi wa kike wa kanisa hilo akiachwa na mshale mgongoni.

Akiongea na waandishi wa habari, Kalul aliaani vikali kisa hicho akisema kikosi pinzani kilitaka kumpaka tope ili aonekane kama mtu wa kupenda fujo. Kikosi chake kilidai Adika ambaye aliwasili kutoka Amoyo ambayo inafananishwa na Yerusalemi kwenye Biblia alinuia kuchukua mabaki ya mwanzilishi wa Got Kwer.