Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju amethibitisha kuondolewa kwa Abdi Guyo kama kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Nairobi. Nafasi yake sasa inachukuliwa na Charles Thuo.
Haya yanajiri siku moja baada ya kushuhudiwa kwa ghasia katika majengo la bunge hilo, baada ya Spika Beatrice Elachi Kutangaza mabadiliko haya. Abdi Guyo aliongoza baadhi ya wawakilishi wadi wanaoegemea upande wa Jubilee kumn’gatua spika wa bunge mwaka moja baada ya kurejeshwa kazini na mahakama ya wafanyikazi nchini Labour Courts.