Wajumbe watano wamerizai wakati wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuruhusiwa kuhudhuria Kongamano kuhusu idadi ya watu. Kongamano hili linaendelea katika jumba la mikutano la kimataifa la KICC.
Maelfu ya wajumbe pia wamekosa nafasi kuhudhuria ufunguzi wa kongamano hilo na matukio ya siku ya Jumanne. Wajumbe hao walisalia kwa muda wa masaa manne kabla ya kukubaliwa kuingia.
Zoezi la uithinishaji iliendeshwa na UNFPA na kampuni mbili za kutoa huduma za uhusiano mwema (PR) nje ya majengo ya bunge la kaunti ya Nairobi. Wajumbe hao watano waliozirahi walipokea huduma ya kwanza nje ya jumba la KICC sehemu ambapo kongamano hilo linaendelea.
Kongamano hilo limefunguliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta