Posted on: November 12, 2019 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Kampuni ya ndege ya Silverstone imesitisha kwa muda safari zake baada ya liseni yake kuondolewa. Wakati huu kampuni hiyo itawasiliana na wateja wake kuzuia mahangaiko zaidi.

Mapema ndege nane za kampuni hiyo zilipigwa marufuku ili kutoa nafasi kwa uchunguzi wa kina wa kile kilichopelekea kusababishwa kwa ajali hivi majuzi.KCAA pia imepiga marufuku huduma za ndege ya SAC inayoendesha biashara ya kubeba mzigo na Alof ambayo husafirisha gesi.