Posted on: January 15, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Rais Uhuru Kenyatta alisitisha utekelezwaji wa masharti mapya ya Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) ili kuruhusu mazungumzo zaidi kati ya washika dau . Amri ya rais aliyoitoa Jumanne, Januari 14, katika Ikulu ya Mombasa iliwadia baada ya Wakenya kulalamika, wakiwemo Muungano wa vyama vya wafanyakazi (COTU) na viongozi kadha kutoka pembe mbalimbali za nchi.

Hazina hiyo ya matibabu ilikuwa imetangaza masharti mapya magumu na miongoni mwayo kupunguza idadi ya wanufaishwa kuwa mke mmoja na watoto watano. Mabadiliko mengine yaliyokuwa yamependekezwa ni wateja wapya kusubiri siku 90 kuanza kupata huduma na pia mteja anahitajika kulipia huduma mwaka mmoja mbele katika kipindi cha kusubiri.

Mwandishi Kevin Oduor