Sunday, May 19, 2024
HomeNewsMan U ndio magojoo wa Manchester

Man U ndio magojoo wa Manchester

Vijana wa kocha Ole Guna Solksjaer, jana usiku waliweza kuwapiku
mahasimu wao wa jadi na majirani wao Mancity kwenye debi iliyotia fora
ughani mwao Old Trafford. Bao la kwanza liliweza kuwekwa kimiani na
mchezaji Anthony Martialy mnamo kwenye dakika ya thelani ya kipindi
cha kwanza baada ya kupata pasi lenye tija za hadhi ya kimataifa
kutoka kwa mchezaji mwenza Bruno Fernandes. Hata baada ya Manchester
City kuweza kuonyesha usogora wao kwenye ulimbwende wa kung’arisha
ving’aring’ari katika ulingo wa soka ya Uingereza na pia kuumiliki
mpira kwa asilimia kubwa kuwashinda Machester United hawakuweza kupata
nafasi za kulishambulia lango la Manu United kwani walinda lango Harry
Maguire, Aaron Wan-Bissaka na Luke Shaw waliweza kuziba kabisa kwa
mikiki ya majabali watu.

Ushindi huu umeiwezesha timu hii ya Manchester United kupanda juu ya
jedwali la ligi kuu ya Uingereza toka nafasi ya saba hadi ya tano
alama tatu nyuma ya Chelsea ambao wako nafasi ya tano kwa alama
arobaini na nane. Mchezaji wa akiba na kinda Scott MC Tominay
aliidhibitishia Manchester United ushindi mnono kwa kutingisha wavu
kwa mara ya pili mnamo kwenye dakika za lala salama. Scott
alivurumisha mkwaju mrefu kwenye hatua ya zaidi ya yadi thelathini na
nane kutoka kwenye lango la Manchester City, katika dakika ya ziada ya
tisini na sita pale mlinda lango wa Mancity Enderson alipojisahau
nakutoka nje ya eneo lake na hatari na kupeana nafasi kwa Scott
kufunga bao zuri sana.

Ushindi wa Manchester United unarejesha imani ya mashabiki kwa
wachezaji ambao kwa mda mrefu wamekua wakiandikisha matokea ambayo
hayatii furaha hata kidogo. Twakimu zinasema kuwa Manchester United
kushindwa na Manchester City wakiwa nyumbani Old Trafford imekuwa
kawaida kwa takriban mda wa muongo mmoja kwasasa. Ila jana Mashetani
hawa wekundu walionyesha makali yao mbele ya mashabiki wao kote
ulimwenguni na kujizatiti kupigania nafasi nne bora za kwanza kwenye
ligi kuu ya Uingereza, ili kuweza kupiga kwenye mashindano ya UEFA
champions mwwakani.

Kamadi Amata
Kamadi Amatahttps://mtaaniradio.or.ke
I am a digital content creator with niche in Health, politics, and Human Interest Features.
RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments

Solverwp- WordPress Theme and Plugin

Facebook

adapazarı escort Eskişehir escort bayan