Posted on: March 10, 2020 Posted by: Kamadi Amata Comments: 0

Mwandishi : Kevin Oduor

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na baadhi ya magavana kutoka mkoa wa Bonde la Ufa katika Ikulu ya Nairobi Mkutano huu umejiri huku kukiwepo na wasiwasi mkubwa wa viongozi kutoka eneo hilo kugawanyika kwa ajili ya mpango wa BBI. Mkutano wa BBI unatarajiwa kufanyika Jumamosi, Mach 21, mjini Nakuru baadhi ya ajenda waliojadili magavana hao ilikuwa ni kuhusu mchakato wa BBI.

Kufuatia taarifa kutoka Ikulu, magavana hao walimhakikishia Uhuru kuwa mkutano huo utakuwa wenye mafanikio makubwa na utaendeshwa kama ilivyoratibiwa. Mkutano huo wa BBI ulikuwa ufanyika Jumamosi, Machi 7, ila ukaharishwa baada ya ule wa Meru kukumbwa na vurugu.